Yesu Kwetu Ni Rafiki

[1]
Yesu kwetu ni rafiki,
Huambiwa haja pia
Tukiomba kwa babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia

[2]
Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia

[3]
Je, hunayo hata nguvu
Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia
Watu wangekudharau,
Wapendao ndunia,
Hukwambata mikononi
Dua atasikia.