Nimekombolewa Na Yesu

[1]
Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.

[chorus]
Kombolewa, kombolewa
Nakombolewa na damu (ya Yesu)
Kombolewa,kombolewa
Mimi mwana wake kweli.

[2]
Kukombolewa nafurahi
Kupita lugha kutamka
Kulionyesha pendo lake
Nimekua mtoto wake.

[chorus]
Kombolewa, kombolewa
Nakombolewa na damu (ya Yesu)
Kombolewa,kombolewa
Mimi mwana wake kweli.

[3]
Nitamwona uzuri wake
Mfalme wangu wa ajabu
Na sasa najifurahisha
Katika neema yake.

[chorus]
Kombolewa, kombolewa
Nakombolewa na damu (ya Yesu)
Kombolewa,kombolewa
Mimi mwana wake kweli.

[4]
Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu

Muda kitambo atakuja
Ili alipo niwepo.

[chorus]
Kombolewa, kombolewa
Nakombolewa na damu (ya Yesu)
Kombolewa,kombolewa
Mimi mwana wake kweli.