Peleleza Ndani Yangu

[1]
Peleleza ndani yangu, iwe safe nia,
Kwangu kama kwako Mungu, idhihiri pia

[2]
Peleleza moyo wangu, unifunulie
Yaliyomo ndani yangu, nami niyajue.

[3]
Kwanza osha dhambi zako, kumefunga giza
Nijue ambavyo dhambi, niza kuchukiza.

[4]
Peleleza na mawazo, ni mbegu za mambo
Asili ya machukizo, maumbuo-umbo.

[5]
Zidi kuyapeleleza, katikati yangu,
hata mwisho, nifundishe udhaifu wangu.

[6]
Hapo nikikwinamia mbele yako Mungu,
Hakika nitakujua, U mpenzi wangu.