Umoja

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Umoja

[1]
Mungu Baba na Yesu Kristo
Wako na umoja
Uzima hupatikana kwao
Ndio wenye mapenzi

[chorus]
Kweli:
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi

[2]
Salamianeni wote wandugu
Na wadada na wamama
Tusalamianeni Wakristo
Katika jina la Kristo

[chorus]
Kweli:
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi

[3]
Paulo na Barnaba walipo
Rudi kule Antiokia
Waliwaeleza Wakristo
Aliyoyafanya Mungu

[chorus]
Kweli:
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi

[4]
Mungu ametuunganisha
Na Wakristo wenzetu
Kwa kuihubiri injili
Na kusalamiana

[chorus]
Kweli:
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi
Rehema na neema na amani
Zitakuwa pamoja nasi