Nitaongozwa Na Bwana

[1]
Aniongoza po pote
Nimwandame siku zote
Kwa ajili yangu mimi
Aliuwawa kalvari

[Chorus]
Nitaongozwa na Bwana,
Usiku kucha na mchana
Yesu rafiki wa heri,
Ninakumbuka kalvari

[2]
Lanitosha neno lake
Nishikwe na mkono wake
Mapenzi yake ni heri
Yalitimizwa kalvari

[3]
Nitaendelea mbele
Pamoja naye milele
Pendo lake ni hiari
Bwana Yesu wa Kalvari