Twende Kwa Yesu

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Twende Kwa Yesu

[1]
Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia atwonya tuijue
Imo chuoni na mwenyewe
Hapa asema, njoo!

[chorus]
Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako mwokozi kuonana,
Na milele kukaa.

[2]
"Wana na waje" atwambia
Furahini mkisikia
Ndiye mfalme wetu pia
Na tumtii,njoo!

[chorus]
Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako mwokozi kuonana,
Na milele kukaa.

[3]
Wangojeani? Leo yupo:
Sikiza sana asemapo,
Huruma zake zikwitapo,
Ewe kijana, njoo!

[chorus]
Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako mwokozi kuonana,
Na milele kukaa.