AFUNGULIWE NANI?

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

AFUNGULIWE NANI?

[1]
Afunguliwe nani, Baraba au Yesu.
Walijibu upesi sana, afunguliwe Baraba

Yesu, Yesu asulubiwe, Baraba yeye awe huru, x2
Pilato alinawa mikono.
Mbele yao wale makuhani.

[2]
Kapigwa mijeredi, kasokotewa taji,
Alitemewa mate “Yesu”, ili niokolewe.

[3]
Wengi walitania, aokoa wengine
Yeye hajiokoi, anamwita Eliya.

[4]
Ni ushindi wa Yesu, ufuni kafufuka
Nchi katetemeka, Ukombozi tayari.