Tazama Kule Kalvari

[1]
Tazameni kule kalvari
Mwokozi aliteswa na dhambi
Alizikwa kule kaburini
Mwishowe akatoka kwa ushindi

[chorus]
Nitashinda nitashinda
Kama wewe pia ulishinda
Nitapita mapitoni mwako
Oh nimeanza Bwana nitashinda

[2]
Njia mbofu zote nimeacha
Nitapita njia nyembamba
Walipita Elia na Musa
Walianza Bwana wakashinda

[chorus]
Nitashinda nitashinda
Kama wewe pia ulishinda
Nitapita mapitoni mwako
Oh nimeanza Bwana nitashinda

[3]
Kupokea nyimbo za ushindi
Uliinuliwa kwa mawingu
Malaika kutwa wanaimba
Wanasifu nyimbo za ushindi

[chorus]
Nitashinda nitashinda
Kama wewe pia ulishinda
Nitapita mapitoni mwako
Oh nimeanza Bwana nitashinda