Ni Mwokozi Aliyenifia

[1]
Ni Mwokozi aliyenifia,
nitoke dhambini alisema
Yeye aliyemwamini mwana,
anao uzima

[chorus]
Amini, amini nakuambia
Amini, amini ujumbe mpya
Yeye aliyemwamini Mwana,
anao uzima.

[2]
Dhambi zangu zilichukuliwa,
Deni zangu zote zililipwa
Wote waliomwamini Mwana,
Wanao uzima

[chorus]
Amini, amini nakuambia
Amini, amini ujumbe mpya
Yeye aliyemwamini Mwana,
anao uzima.

[3]
Ijapo ningekuwa maskini,
Ijapo ningekuwa mkosaji
Neno la furaha la mwokozi,
Ninao uzima

[chorus]
Amini, amini nakuambia
Amini, amini ujumbe mpya
Yeye aliyemwamini Mwana,
anao uzima.

[4]
Na sina shaka, nitamwamini,
Yeye ajaye kwake hatupwi
Amwaminiye, tuma habari,
Tunao uzima.

[chorus]
Amini, amini nakuambia
Amini, amini ujumbe mpya
Yeye aliyemwamini Mwana,
anao uzima.