Sioni Haya Kwa Bwana

[1]
Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang'ara, mtiwake sitakana
Ni neno imara

[chorus]
Msalaba ndio asili ya mema
Nitatua mzigo hapo
Nina uzima, furaha daima
Njooni kafurahini papo

[2]
Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi,alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.

[chorus]
Msalaba ndio asili ya mema
Nitatua mzigo hapo
Nina uzima, furaha daima
Njooni kafurahini papo

[3]
Bwana Wangu,tena Mungu
Ndilo lake jina. Hataacha roho yangu
Wala kunikana

[chorus]
Msalaba ndio asili ya mema
Nitatua mzigo hapo
Nina uzima, furaha daima
Njooni kafurahini papo

[4]
Atakiri langu jina
Mbele za Babaye; Anipe pahali tena
Mbinguni nikae

[chorus]
Msalaba ndio asili ya mema
Nitatua mzigo hapo
Nina uzima, furaha daima
Njooni kafurahini papo