Ni Siku Kuu

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Ni Siku Kuu

[1]
Ni siku kuu siku ile
Ya kumkiri mwokozi
Moyo umejaa tele
Kunyamaza hauwezi

[chorus]
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu
Hukesha na kuomba tu
Ananiongoza miguu
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu

[2]
Tumekwisha kupatana
Mimi wake, yeye wangu
Na sasa nitamwandama
Nikiri neno la Mungu

[chorus]
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu
Hukesha na kuomba tu
Ananiongoza miguu
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu

[3]
Moyo tulia kwa bwana
Kiini cha raha yangu
Huna njia mbili tena
Yesu ndio njia yangu

[chorus]
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu
Hukesha na kuomba tu
Ananiongoza miguu
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu

[4]
Nadhiri yangu ya mbele
Nitaiweka daima
Hata ije siku ile
Ya kuonana kwa salama

[chorus]
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu
Hukesha na kuomba tu
Ananiongoza miguu
Siku kuu, siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu