WATU WA LEO

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

WATU WA LEO

[1]
Watu wa leo wanapotenda dhambi
Wanajipa moyo, wanajifariji
Wasema eti, “sio vibaya,
Nitatenda leo, kesho nitatubu.”

“Nitatubu jioni, nitatubu kesho,
Jumapili nipo, wanajifariji.”

[2]
Vijana nao wanapokwenda disko
Wanajipa moyo, wanajifariji
Wasema, “eti sio vibaya
Nitacheza leo kesho nitatubu.”

[3]
Wazee nao wanapokwenda baa
Wanajipa moyo, wanajifariji
Wasema, “eti sio vibaya kunywa
Mbili tatu bora usilewe.”

[4]
Ninawasihi watu wa dunia
Wamtazame Yesu yeye anatosha
Utubu leo wala sio kesho,
Kesho haifiki wewe unapita.