Wandugu Na Wadada

[1]
Wandugu zetu na wadada wote
Jihadhari siku inayokuja
Siku ile isiyojulikana
Ila Mungu pekee ajuaye

[chorus]
Wenye dhambi, wote watalia
Watakapotupwa motoni
Watalia woi, woi, woi, woi,
woi, woi kama tungejua

[2]
Waliookoka watapokelewa
Kwa imani watamtumikia
Bwana Yesu atawakaribisha
Kwa ulinzi wa ufalme wa mbinguni

[chorus]
Wenye dhambi, wote watalia
Watakapotupwa motoni
Watalia woi, woi, woi, woi,
woi, woi kama tungejua

[3]
Watu watatoa visababu
Wengine watasema ni wahubiri
Wengine watasema ni wakanisa
Na Mungu Baba hatawasikiliza

[chorus]
Wenye dhambi, wote watalia
Watakapotupwa motoni
Watalia woi, woi, woi, woi,
woi, woi kama tungejua

[4]
Wahubiri walihubiri
Bibilia inasema wazi
Jihadhari mlango utafungwa
Ukibisha utafunguliwa.

[chorus]
Wenye dhambi, wote watalia
Watakapotupwa motoni
Watalia woi, woi, woi, woi,
woi, woi kama tungejua