Waimba Sikizini

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Waimba Sikizini

[1]
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni,
Wimbo wa tamu sana, wa pendo zake Bwana,
"Duniani salama, Kwa wakosa rehema"
Sisi sote na twimbe, nao wale wajumbe,
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni

[2]
Ndiye Bwana wa mbingu, Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwili;
Ametoka enzini, Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie, ili tusipotee
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.

[3]
Seyidi wa amani, Ametoka mbinguni,
Jua na haki, ndiye atumulikiaye
Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi
Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya,
Waimba, sikizeni, Maliika mbinguni

[4]
Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana;
Kaa nasi, Mwokozi, Vita hatuviwezi,
Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika,
Tufanane na Wewe, Kwetu sifa upewe
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.