Wachunga Walipolinda

[1]
Wachunga walipolinda, kucha nyama zao,
Malaika mtukufu, Alishuka kwao
Wakacha sana wachunga, Akawatuliza,
"Nawaletea habari ya kupendeza".

[2]
" Mji ule wa Daudi, Leo amezawa
Mwokozi, ni Kristo Bwana, Iivyoandikwa:
Huyo Mwana wa mbinguni, Ataonekana,
Amelazwa kihorini, Malazi hapana".

[3]
Alipokwisha yanena, Malaika hao
Waliimba wimbo huu, Usio na mwisho;
"Enzi ni yake Mungu juu. Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima".