UFUNUO WA YOHANA

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

UFUNUO WA YOHANA

[1]
Ufunuo wa Yohana akiwa kisiwani (Patimo)
Kaonyeshwa kaiona hukumu imefika (jamani).

[chorus]
Bwana ameketi na yuko tayari kuwahukumu
Amekishika na kile kitabu cha uzima,
Anasoma nani ameandikwa.
Wale wasioandi kwa watalia sana
Kusukumwa Jehanamu.
Jehanamu (x2) -(humo, humo, humo),
Jehanamu ni mateso.
Jiulize kama ndugu umeisha andikwa
Usiende Jehanamu -watalia “sana”
Watalia “sana” kusukumwa Jehanamu.

[2]
Na tazama aliona dunia inatupwa (motoni)
Jina lake aliitwa Alfa na Omega (jamani).

[3]
Ndugu yangu wasemaje Yesu anakuita (kimbia)
Usingoje kuambiwa miango utafungwa (kimbia).