Twendeni Askari

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Twendeni Askari

[1]
Twendeni askari, watu wa mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.

[chorus]
Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;

[2]
Jeshi la shetani, likisikia
Jina la mwokozi, litakimbia,
Kelele za shangwe zivume nchi;
Ndugu inueni zenu sauti.

[chorus]
Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;

[3]
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu.
Sisi na mababa tu moja fungu
Hatutengwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.

[chorus]
Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;

[4]
Haya mbele watu nasi njiani.
Inueni mioyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.

[chorus]
Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;