Tunayo Safari

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Tunayo Safari

[1]
Tunayo safari ya kwenda
Mbinguni, mbinguni kwa Baba
Tunayo safari ya kwenda
Mbinguni, mbinguni, kwa Baba

[Chorus]
(Njiani) Kuna vikwazo vinavyokwaza watu
(Visiki) Na makonge ya kuangusha wengi
(Ni nani) Awezaye kutuondolea yote
(Hakuna) Mwingine ila Yesu Mwokozi

[2]
Safari ni ndefu ya kwenda
Mbinguni, na tena ni ngumu
Safari ni ndefu ya kwenda
Mbinguni, tena ni ngumu

[Chorus]
(Njiani) Kuna vikwazo vinavyokwaza watu
(Visiki) Na makonge ya kuangusha wengi
(Ni nani) Awezaye kutuondolea yote
(Hakuna) Mwingine ila Yesu Mwokozi

[3]
Ulevi, uzinzi, uongo na chuki
Visiki na makonge njiani
Ulevi, uzinzi uongo na chuki
Visiki na makonge njiani

[Chorus]
(Njiani) Kuna vikwazo vinavyokwaza watu
(Visiki) Na makonge ya kuangusha wengi
(Ni nani) Awezaye kutuondolea yote
(Hakuna) Mwingine ila Yesu Mwokozi

[4]
Visiki ni dhambi makonge ni
Dhambi tujihadhari zote.
Visiki ni dhambi makonge ni
Dhambi, tujihadhari zote.

[Chorus]
(Njiani) Kuna vikwazo vinavyokwaza watu
(Visiki) Na makonge ya kuangusha wengi
(Ni nani) Awezaye kutuondolea yote
(Hakuna) Mwingine ila Yesu Mwokozi