TULISHITAKIWA WOTE

[1]
Tulishitakiwa wote mahakamani
Na jaji aliamua tunyongwe wote,
Ni Yesu Mwokozi katuhurumia,
Kisha faili kalibeba, kaenda nalo Goligota.

Yesu aliyafuta maandishi ya hukumu,
Kwa damu yake mwenyewe. x2
“Furaha, furaha, tukaachiliwa huru!” x2
Ilikuwa mkikimkiki siku ile, ya kufa Yesu.
Na tetemeko, likatetemeka miamba ikapasuka.
Pilika zake Shetani siku ile zilikomeshwa,
Na mwanadamu akapata uzima ule wa milele.

[2]
Bwana Yesu awaita wafungwa wote,
Deni lenu Iimelipwa msalabani,
Njooni kwangu nyote, nmaosumbuka,
Deni lenu limelipwa, njooni kwangu mpumzike.