TUKUMBUKE SIKU

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

TUKUMBUKE SIKU

[1]
Tukumbuke siku za zamani wale malaika,
Walifika nyumbani kwa Lutu na wakamwambia,
Uondoke nchi hii.
Sodoma, uende nchi nyingine haraka
Naye Lutu kweli kaondoka kwenda.

Na siku hizi - Twazilinganisha
Siku - siku zake Lutu
Watu - Walipenda dunia
Tena - Na kumdharau
Yule - Baba wa Mbinguni
Aliwateketeza wote.

[2]
Ndiyo hapo mke wa Lutu
Aliyegeuka, alipogeuka
Nyuma yake akangamia,
Sababu alikumbuka Sodoma.
Nasi ndugu tusiangalie nyuma.

[3]
Jiulize leo ndugu yangu ujipeleleze,
Wakati huu ni wa kutubu hivyo uelewe,
Utakuja kupoteza uzima,
Utakuwa kama mke wa Lutu
Leo ndugu yangu umwamini Bwana.