SIMONI

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

SIMONI

[1]
Simoni alikuwa mvuvi wa samaki.
Yesu akamwita nifuate.
Aliziacha nyavu, pia na chombo chake.
Kisha kamfuata Bwana Yesu.

Simoni, Simoni aliviacha vyote
Akamfuata Bwana Yesu
Yesu akamwambia
Yesu akamwambia
Ee Simoni ee wewe usiogope
Utakuwa ni mvuvi wa watu.

[2]
Nawe mwenzangu leo Yesu anakuita
Uache ya dunia mfuate
Acha kutangatanga pia dhambi zako
Uje umfuate Bwana Yesu.