Simama Imara

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Simama Imara

[1]
Milima yote na mabonde itayeyuka,
Neno lake Bwana imara litasimama.

[chorus]
(Simama)simama imara jilinde
Neno lake Bwana imara,
Kesha kila siku uombe
(uombe) utasimama X2

[2]
Mapendo ya Mungu tumejaa,
Roho wa kweli.
Imara yetu ndani yake,
Awe muhuri

[chorus]
(Simama)simama imara jilinde
Neno lake Bwana imara,
Kesha kila siku uombe
(uombe) utasimama X2

[3]
Siku za huduma ni chache,
Tuwe mashujaa,
Roho wa Yesu akae nasi,
Mpaka hatima

[chorus]
(Simama)simama imara jilinde
Neno lake Bwana imara,
Kesha kila siku uombe
(uombe) utasimama X2

[4]
Katika yote tutashinda,
Kwa nguvu yake,
Nani aweza kututenga,
Na pendo lake

[chorus]
(Simama)simama imara jilinde
Neno lake Bwana imara,
Kesha kila siku uombe
(uombe) utasimama X2