SIKU ILE

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

SIKU ILE

[1]
Siku ile I karibu (I karibu).
Tarumbeta itakapolia,
Dunia itageuka (itageuka),
Wakosefu watakapolia.

[CHORUS]
Kweli -Watu wa dunia watakuja hukumiwa,
Kweli -Wafikapo mbele ya kiti cha hukumu,
Kweli -Wakosefu watadai kuokolewa,
Kweli -Mwokozi atawambia ondoka, kweli ondoka.

[2]
Siku ile walevi (na walevi),
Watakutwa wakilewa pombe,
Wapigaji wa marimba (Wa marimba), Watakutwa wakicheza dansi.

[3]
Ndugu leo jiulize (jiulize),
Siku ile utakuwa wapi?
Ndugu sasa tubu dhambi (tubu dhambi),
Upate kuingia Mbinguni.