SAUTI YA MUNGU BABA

[1]
Sauti ya Mungu Baba, inaniambia mimi,
Nikifanya dhambi moto uko mbele Yangu mimi, nitalia na kusaga meno.

Ukilewa - Baba kwenye moto
Ukiiba - Mama kwenye moto
Ukiua - Kaka kwenye moto
Uasherati - Dada kwenye moto,
Wa milele.

Walioamini watakuwa “kweli na”
Wakiimba wimbo mtakatifu,
(Wamwimbia Bwana)
Walioamini watakuwa “kweli na”
Wakiimba wimbo mtakatifu
(kwa furaha kubwa)
Walioamini watakuwa “kweli na”
Wakiimba wimbo mkatifu
(wako kwenye viti)
Walioamini watakuwa “kweli na”
Wakiimba wimbo mtakatifu
(Haleluya Bwana)
Walioamini watakuwa “kweli na”
Wakiimba wimbo mtakatifu
“Kweli” Bwana asifiwe.

[2]
Ni wakati wako ndugu wa kutubu dhambi zako,
Ujue unangojewa na hukumu I karibu,
Utalia na kusaga meno.