SASA WAMWITEJE?

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

SASA WAMWITEJE?

[1]
Sasa wamwiteje bila kumwamini?
Na wamwaminije bila mhubiri?
Na wahubirije pasipopelekwa? Na wapelekwaje pasipojitoa?

Kwa maana kila atakayelitia,
Jina lake Yesu ataokoka.
A ache maovu ajitakase,
Ataingia lango la Mbinguni.

[2]
Waamini, Je! Wanaposhuhudia?
Matendo yako kuwa mabaya sana?
Waamini, Je! Wanapoona kuwa, matendo yako kinyume na Injili?

[3]
Tumetangulia kubeba mizigo,
Kuwaleta watu waje kwa Mwokozi
Tuwe wanyeyekevu tena
Wapole, tuwalete wote kwa Mwokozi Yesu.