Sasa Ndio Wakati

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Sasa Ndio Wakati

[1]
Sasa ndio wakati wakutoa sadaka,
Kila mtu aanze, kujifikiria

[chorus]
Toa ndugu, Toa dada
Toa ndugu, Toa dada
Ulicho nacho wewe
Bwana anakuona
Mpaka moyoni mwako

[2]
Wiki nzima Bwana Mungu, alikulinda vyema
Sasa nawe Ndugu yangu ujifikirie

[chorus]
Toa ndugu, Toa dada
Toa ndugu, Toa dada
Ulicho nacho wewe
Bwana anakuona
Mpaka moyoni mwako

[3]
Kumbuka jinsi Yesu alivyojitolea
Pale msalabani kwa ajili yetu

[chorus]
Toa ndugu, Toa dada
Toa ndugu, Toa dada
Ulicho nacho wewe
Bwana anakuona
Mpaka moyoni mwako

[4]
Tolea moyo wako, pia matendo yako
Naye Bwana Mungu atakubariki

[chorus]
Toa ndugu, Toa dada
Toa ndugu, Toa dada
Ulicho nacho wewe
Bwana anakuona
Mpaka moyoni mwako

[5]
Baraka zake Mungu, za Baba na za Mwana
Za Roho Mtakatifu, zikae nanyi nyote

[chorus]
Toa ndugu, Toa dada
Toa ndugu, Toa dada
Ulicho nacho wewe
Bwana anakuona
Mpaka moyoni mwako