PETRO NA YOHANA

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

PETRO NA YOHANA

[1]
Yule Petro pia Yohana
Walikuwa pamoja (wote) Walikwea na kwenda kusali,
Walimwona kiwete (yule)

[chorus]
Alipokwisha waona (wao)
Aliwakazia macho (sana)
Akiomba na apewe (yeye)
Cho chote walicho (nacho). x2
Sisi hatuna dhahabu (kweli)
Hata nayo fedha (ndugu),
Kwa jina la Bwana Yesu
Simama uende. x2
Ilikuwa ajabu (sana)
Kiwete akitembea. x4

[2]
Mara kiwete akasimama,
Akiruka jamani (kweli),
Akaingia kwenye hekalu,
Akimsifu Mungu (Baba).