Panda Asubuhi

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Panda Asubuhi

[1]
Panda asubuhi mbegu ya fadhili
Panda adhuhuri, tena jioni
Tutaingojea siku ya mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno

[chorus]
Leta mavuno, leta mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno X2

[2]
Napanda mwangani, tena kivulini
Usiwe na hofu kwa baridi mkuu
Namwisho wa kazi kuvuna mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno

[chorus]
Leta mavuno, leta mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno X2

[3]
Mvunieni Bwana kwa machozi mengi
Ijapo twaona taabu nyingi
Mwisho wa kilio tutakaribishwa
Tutafurahi kuleta mavuno

[chorus]
Leta mavuno, leta mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno X2