ONDOKA UKATANGAZE

[1]
Ondoka ukatangaze Neno la Mungu
Saa ndiyo hii usichelewe,
Sikia Yesu anakuita,
Ufanye kazi Shambani mwake,

Tazameni-mavuno ni mengi
Jambo moja-mavunaji wachache
Hivyo ndugu-ondoka ingia
Shambani, ili ukavune mavuno
Karibu Bwana Yesu.
Atakuja-kuzichukuwa mbegu Ghalani, karibu Bwana Yesu.

[2]
Katika shamba la Bwana kuna magugu,
Yatakusanywa siku ya mwisho,
Nayo magugu ni baadhi ya watu,
Wapotezao neno la Mungu.