Nitwae Hivi Nilivyo

[1]
Hivi nilivyo kipovu,
masikini na mpungufu,
Wewe umtimilifu,
Bwana Yesu naja, naja

[2]
Nawe hivi utanitwaa,
Nisithubutu kukawa.
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu,naja, naja

[3]
Hivi nilivyo mapenzi
Yamenipa njia wazi,
hali na mali sisazi,
Bwana Yesu naja,naja

[4]
Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu naja,naja

[5]
Hivyo nilivyo si langu,
Kujiosha roho yangu
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu naja, naja;

[6]
Hivi nilivyo sioni,
Kamwe furaha moyoni
Daima ni mashakani
Bwana yesu naja,naja;