NIPITAPO MAJARIBU

[1]
Nipitapo majaribu, katikati ya miiba,
Ninatosheka kwa kuwa, unanifikiri.

Unanifikiri mimi, waniwaza sana Bwana:
Nahitaji kitu gani? Wewe wanitosha.

[2]
Masumbufu ya dunia yasongayo moyo wangu,
Mwisho yananikumbusha, unafikiri.

[3]
Shida zije, maisha bora au ya shida.
Mwisho yananikumbusha, unafikiri.