Niongoze, Bwana Yesu

[1]
Niongoze, Bwana Mungu,
Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, nguvu sina;
Nishike mkononi;
U mkate wa mbinguni
Nilishe siku zote.

[2]
Kijito cha maji mema
Kitokacho mwambani,
Nguzo yako, moto wingu
Yaongoza jangwani,
Niokoe mwenye nguvu;
Nguvu zangu na ngao.

[3]
Nikikaribia kufa,
Sichi neno lo lote,
Wewe kifo umeshinda
Zinawe nguvu zote,
Tutaimba sifa zako,
Kwako juu milele.