Mteteeni Yesu

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Mteteeni Yesu

[1]
Mteteeni Yesu,mlio askari,inueni beramu, mkae tayari
Kwenda naye vitani, sisi hatuchoki, hata washindwe pia
Yeye amiliki

[2]
Mteteeni Yesu, vita ni vikali,leo siku ya Bwana
Atashinda kweli, waume twende naye, adui ni wengi
Lakini kwake Bwana, tuna nguvu nyingi

[3]
Mteteeni Yesu, wenye ushujaa,nguvu zenu za mwili
Hazitatufaa, silaha ya injili, vaeni daima
Kesheni mkiomba, sirudini nyuma

[4]
Mteteeni Yesu,vita ni vikali,wengi wamdharau
Hawamkubali, ila atamiliki, tusitie shaka, kuwa naye vitani
Twashinda hakika