Nionapo Mti Bora

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Nionapo Mti Bora

[1]
Nionapo mti bora,
Kristo aliponifia
Kwangu pato ni hasara
Kiburi nakichukia.

[2]
Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa mauti yako;
Upuzi sitaki tena,
Ni chini ya damu yako

[3]
Tangu kichwa hata nyayo
Zamwagwa pendo na hamu
Ndako pweke hamu hiyo,
Pendo zako zimetimu.

[4]
Vitu vyote vyo dunia,
Si Sadaka ya kutosha,
Pendo zako zaniwia
Nafsi, mali, na maisha.