Nina Haja Nawe

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Nina Haja Nawe

[1]
Nina haja nawe kila saa:
Hawezi mwingine kunifaa.

[Chorus]
Yesu nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia,

[2]
Nina haja nawe; kaa nami,
Na maonjo haya, Hayaumi.

[Chorus]
Yesu nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia,

[3]
Nina haja nawe: Kila hali,
Maisha ni bure, Uli mbali.

[Chorus]
Yesu nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia,

[4]
Nina haja nawe, Nifundishe
Na ahadi zako zifikishe.

[Chorus]
Yesu nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia,

[5]
Nina haja nawe; Mweza yote
Ni wako kabisa siku zote.

[Chorus]
Yesu nakuhitaji,
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi, Nakujia,