Nimelemewa Na Hatia Zangu

[1]
Nimelemewa na hatia zangu
Nakutamani kufikia mbingu
Ingawa mwenye dhambi haingii
Iko sauti yaniita nije.

[chorus]
(Naja) Naja kwako Yesu Bwana
(Nisa) Nisafiwe dhambi zangu X2

[2]
Mimi mchafu nitaweza wapi
Kufika kwenye nchi takatifu
Kitini kwa mwamuzi nisimame
Uko mkono wanivuta nije.

[chorus]
(Naja) Naja kwako Yesu Bwana
(Nisa) Nisafiwe dhambi zangu X2

[3]
Ingawa natamani kufuata
Njia ya haki dhambi zanipinga
Lakini nasikia neno njema
Tubu ungama utasamehewa.

[chorus]
(Naja) Naja kwako Yesu Bwana
(Nisa) Nisafiwe dhambi zangu X2

[4]
Sauti yako Yesu nasikia
Mikono yake yanivuta leo
Na damu yako yanisafisha dhambi
Na kuniweka safi mbele yako.

[chorus]
(Naja) Naja kwako Yesu Bwana
(Nisa) Nisafiwe dhambi zangu X2