Nilipotea Na Kutangatanga

[1]
Nilipotea na kutangatanga
Kwenye bahari ya dhambini
Bwana Yesu aliniita nyumbani
Nikae kwake salama.

[chorus]
Nimo safarini nimetia nanga
dhambini sitarudi tena
Hata pepo na dhoruba zikivuma
Kwake Yesu niko salama

[2]
Namsifu Yesu ameniokoa
Namwimbia kwa furaha
Yesu pekee mwokozi wa ulimwengu
Kimbilio,ngome, bandari.

[chorus]
Nimo safarini nimetia nanga
dhambini sitarudi tena
Hata pepo na dhoruba zikivuma
Kwake Yesu niko salama

[3]
Ni wa salama huyu Bwana yesu
Tumaini la hakika
Mikononi mwake hakuna shaka
Kimbilio, ngome, bandari.

[chorus]
Nimo safarini nimetia nanga
dhambini sitarudi tena
Hata pepo na dhoruba zikivuma
Kwake Yesu niko salama

[4]
Njoo kwa mwokozi anakungojea
Akuokoe kabisa
Kimbilia leo kituoni mwake
Uwe wake hata milele

[chorus]
Nimo safarini nimetia nanga
dhambini sitarudi tena
Hata pepo na dhoruba zikivuma
Kwake Yesu niko salama