NDUGU SIKIA

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

NDUGU SIKIA

[1]
Ndugu sikia, nimeamua ee kuwa na Yesu
Moyoni mwangu, nakushauri nawe amua ee,
Kuwa na Yesu moyoni mwako.

Dunia: Dunia hii matatizo,
Dunia hii mahangaiko,
Dunia hii inapita,
Kiburi chake kinapita,
Imelemewa na utumwa.

[2]
Ndugu sikia kurudi kwake ee, Mwana wa
Mungu kwa karibia, ujiulize kama u-tayari ii,
Kwenda na Yesu kule Mbinguni.

[3]
Dunia hii, dunia hii ii, yawayawaya kama
Machela, dunia hii, dunia hii ii.
Yalewalewa kama mlevi.