Ndiyo Dhamana Yesu Wangu

[1]
Ndiyo dhamana Yesu wangu
hunipa furaha za mbingu
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa kwa Roho yake

[chorus]
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu

[2]
Kumsalimu moyo wangu
Mara namwona raha yangu
Aniletea malaika
Wananilinda taokoka

[chorus]
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu

[3]
Sina kinyume nashukuru
Mchana kutwa huja kwangu
Usiku kucha kuna nuru
Mwokozi wangu ndimi huru

[chorus]
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu

[4]
Hali na mali anitwaa
Mara namwona anifaa
Nami nangoja kwa subira
Akiniita nije mara

[chorus]
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu
Habari njema raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu