NASIKITIKA NDUGU

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

NASIKITIKA NDUGU

[1]
Nasikitika ndugu na dunia hii (ilivyokwisha)
Ilivyokwisha haribika (maovu)
Maovu mengi yanazidi (kuja)
Kuja kwa Bwana ni karibu.

Utafanya nini Bwana akirudi x2
Utalia tena utasumbuka x2
Na mwisho Bwana - Mwisho Bwana,
Atasema - Atasema,
Siwajui ninyi ondoka.

[2]
Na sasa ndugu yangu tufanye kazi
Talanta zetu tuzalishe
Makao yetu ya milee (jina)
Jina la Bwana litukuzwe.

[3]
Safari yetu ndugu kwenda mbinguni
Kwenye makao ya milele (kuna)
Kuna uzima wa milele (kwao)
Kwao waaminio wokovu.