Mwokozi Moyoni Mwangu

[1]
Tangu siku hiyo aliponijia
Akae moyoni mwangu
Sina giza tena ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu

[chorus]
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

[2]
Sina haja tena ya kutangatanga
Ndiye kiongozi wangu
Dhambi zangu zote zimeondolewa
Kwa Yesu Mwanawe Mungu

[chorus]
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

[3]
Matumaini yangu ni ya hakika
Katika mwokozi wangu
Hofu yangu na hamu zimeondoka
Kwa kuwa ninaye Yesu.

[chorus]
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

[4]
Siogopi tena nikiitwa kufa
Yu nami daima Yesu
Mlango wa mbinguni ni yeye pia
"Tapita humo kwa damu".

[chorus]
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.

[5]
Nitaketi na Yeye huko milele
Nisifu mwokozi wangu
Nina raha moyoni majira yote
Kwa Yesu Mwanawe Mungu.

[chorus]
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye
Yu nami moyoni mwangu.