Mungu Yuko Nasi Hapa

[1]
Mungu yuko nasi hapa
Kwa Roho kutufufua
Tazameni mawinguni
Yako karibu kunyesha.

[chorus]
Tunyeshewe twakuomba
Umande wenye baraka
Twangojea,twangojea
Ufufue mioyo yetu.

[2]
Mungu yuko nasi hapa
Mioyo yetu imemwona
mioyo yetu itukuzwe
kwa hiyo neema yako.

[chorus]
Tunyeshewe twakuomba
Umande wenye baraka
Twangojea,twangojea
Ufufue mioyo yetu.

[3]
Mungu yuko nasi hapa
Haja zetu twazileta
Upendo wake uwashe
Mioyo zetu iwakishwe.

[chorus]
Tunyeshewe twakuomba
Umande wenye baraka
Twangojea,twangojea
Ufufue mioyo yetu.

[4]
Mwokozi utusikie
Maombi yetu tupewe
Yafungue madirisha
Tupate kubarikiwa.
[chorus]
Tunyeshewe twakuomba
Umande wenye baraka
Twangojea,twangojea
Ufufue mioyo yetu.