Mungu Mtukufu Aliye Bwana

[1]
Mungu mtukufu aliye Bwana
Akamtoa Yesu mpendwa mwana
Akawa dhabihu kwa dhambi zote,
Kufungua njia kwa watu wote

[Chorus]
Msifuni, msifuni, Nchi imsikie;
Msifuni, msifuni, Bwana Mshangilie
Njooni kwake Baba, Kwa Yesu Mwana,
Mpeni heshima, Aliye Bwana

[2]
Ukombozi wetu, tendo la Mungu
Ni ukamilifu kwa kila mtu;
Mwenye ukosefu akimwamini
Atasamehewa na Yesu, kweli

[Chorus]
Msifuni, msifuni, Nchi imsikie;
Msifuni, msifuni, Bwana Mshangilie
Njooni kwake Baba, Kwa Yesu Mwana,
Mpeni heshima, Aliye Bwana

[3]
Ametufundisha mambo ya mbingu
Tukafurahishwa na Mwana Mungu
Ametuinua tukae naye
Atatuongoza hata milele.

[Chorus]
Msifuni, msifuni, Nchi imsikie;
Msifuni, msifuni, Bwana Mshangilie
Njooni kwake Baba, Kwa Yesu Mwana,
Mpeni heshima, Aliye Bwana