MTU MMOJA HAWEZI

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

MTU MMOJA HAWEZI

[1]
Mtu mmoja hawezi Lazaro mwenye mji,
Mariamu pia Martha hao ni dada zake.

[chorus]
Ugonjwa hata mauti, Yesu kaja kaita,
Lazaro we Lazaro, fufuka tuonane.

[2]
Dada zake Lazaro walianza kulia,
Lololo e lololo kaka yetu amekufa

[3]
Basi Wayahudi wote walifanya shauri,
La kumwua Bwana Yesu kwa kuwa kafufua.