MPANZI MMOJA

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

MPANZI MMOJA

[1]
Mpanzi mmoja alitoka kupanda mbegu njema,
Adui naye akaja kupanda magugu
Mbegu zote zikawa zimechanganyikana, x2
Kwa pamoja,

[chorus]
Ooh! -watumwa wake,
Mwenye myumba -wakamwambia
Bwana tunataka -tukayang’oe,
Magugu shambani -Magugu yote
Bwana kawambia -Acheni yote
Yakue pamoja -Mpaka mwisho
Siku ya mavuno -Na wavunaji
Ni malaika -Ni malaika

[2]
Azipandaye mbegu njema ni Mwana wa Adamu,
Mbegu njema ni neno lake Mungu Baba,
Na yale magugu ni wana wa mwovu Shetani, x2
jihadharini.

[3]
Shamba lake Mungu Baba ni ulimwengu huu,
Na mbegu njema ni neno la Ufalme wa Mungu
Yatupasa kuzaa matunda mazuri, x2
Siku zote.