Mji Wa Yerusalemu

[1]
Mji wa Yerusalemu umetayarishwa sana
Milango kumina mbili ya watu wa Mungu
Imeandikwa majina ya wateule wake Mungu
Majina hayo kabila ya Waisraeli.

[chorus]
Upande - Upande wa mashariki milango mitatu
Upande - Upande wa magharibi milango mitatu
Kusini - kusini kasikazini mitatu mitatu
Zitaingia kabila ya Waisraeli.

[2]
Yesu atakaporudi kuchukua wateule
Wengine watakimbia tena siku hiyo
Majeshi ya mia moja arobaini na nne elfu
Wataimba Halleluyah na mwana kondoo

[chorus]
Upande - Upande wa mashariki milango mitatu
Upande - Upande wa magharibi milango mitatu
Kusini - kusini kasikazini mitatu mitatu
Zitaingia kabila ya Waisraeli.