Mji Mzuri

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Mji Mzuri

[1]
Kuna mji mzuri Jerusalem,
Uliopambwa hasa kwa kila rangi
Uliotayarishwa na kubaliwa,
Na watakaoshinda dhambi milele [X2]

[chorus]
Umejengwa, na Mungu,
Naye mwana kondoo.
Ni mji wa raha, shida magonjwa na
Maombolezo havipo milele.

[2]
Waliokombolewa toka dhambini,
Watakwenda mbinguni Jerusalem
Watafutwa machozi na mwana kondoo,
Wataimba hosana mbele ya Mungu [X2]

[chorus]
Umejengwa, na Mungu,
Naye mwana kondoo.
Ni mji wa raha, shida magonjwa na
Maombolezo havipo milele.

[3]
Katika mji ule Jerusalem,
Hautaingiliwa kamwe na mwovu,
Ole wetu kabisa tusipo shinda,
Hatutakaribishwa Jerusalem [X2]
[chorus]
Umejengwa, na Mungu,
Naye mwana kondoo.
Ni mji wa raha, shida magonjwa na
Maombolezo havipo milele.