Mimi Ndiye Wa Kwanza

[1]
Mimi ndiye wa mwanzo, tena na wa mwisho
Usiwe naye Mungu, mwingine kabisa.
Ndivyo anavyosema, bwana wa majeshi,
Mungu mtakatifu, mwenye nguvu zote.

[chorus]
Mimi nitampa ( yule) ahadi ya uzima (bure)
Yule atakayeshinda ya dunia hayo (yote)
Atakuwa ndani yangu hata mimi ndani yake,
Kwenye utukufu ule, wataimba juu mbinguni

[2]
Mimi nilikuumba unitumikie
Katika siku zote hapa duniani,
Mbona sasa waacha njia ile nzuri,
Wamfuata shetani atakupoteza.

[chorus]
Mimi nitampa ( yule) ahadi ya uzima (bure)
Yule atakayeshinda ya dunia hayo (yote)
Atakuwa ndani yangu hata mimi ndani yake,
Kwenye utukufu ule, wataimba juu mbinguni

[3]
Wacha udanganyifu twende kwake sasa
Yeye ni wa rehema tena wa upole,
Machozi yetu yote yeye atafuta
Tutakapomwendea na kutubu kweli.

[chorus]
Mimi nitampa ( yule) ahadi ya uzima (bure)
Yule atakayeshinda ya dunia hayo (yote)
Atakuwa ndani yangu hata mimi ndani yake,
Kwenye utukufu ule, wataimba juu mbinguni