MBINGUNI KWA BABA

[1]
Mbinguni kwa Baba (yangu), makao ni mengi (sana)
Nakwenda kwa Baba (yangu), njia ninaijua,
(Ya kwenda kwa Baba yangu).

Msalaba wangu (mimi).
Ni njia ya kweli (kweli),
Msalaba wangu (mimi) utanifikisha juu,
Mbinguni kwa Baba (yangu).
Lakini ni njia ya matatizo, kwenda mbinguni
Kwa uwezo wake (Mungu) nitaweza kufika juu,
Mbinguni kwa Baba (yangu).

[2]
Twende kwa Bwana (Yesu), tukiwaza msalaba (ule),
Kwa uwezo wake (Mungu) nitaweza kufika juu,
(Tukiwa na mwili mpya).