Mbele Ninaendelea

[1]
Mbele ninaendelea,
Ninazidi kutembea
Maombi uyasikie
Ee Bwana unipandishe

[chorus]
Ee Bwana niinue
kwa imani nisimame
nipande milima yote
Ee bwana unipandishe

[2]
Sina tamani nikae,
Mahali pa shaka, kamwe
hapo wengi wanakaa,
Kuendelea naomba.

[chorus]
Ee Bwana niinue
kwa imani nisimame
nipande milima yote
Ee bwana unipandishe

[3]
Nasikia duniani
ni mahali pa shetani,
Natazamia mbinguni
Nitafika kwa amani.

[chorus]
Ee Bwana niinue
kwa imani nisimame
nipande milima yote
Ee bwana unipandishe

[4]
Nataka nipandishwe juu
Zaidi yale mawingu
Nitaomba nifikishwe
Ee Bwana unipandishe

[chorus]
Ee Bwana niinue
kwa imani nisimame
nipande milima yote
Ee bwana unipandishe